‘OMO wa ACT hana cha kuzungumza ziarani Uingereza’

0


Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

MAKAMU wa Kwanza wa Rais katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, Othman Masoud Othman ‘OMO’, ambaye yupo ziarani nchini Uingereza anadaiwa kukosa cha kueleza kutokana na kazi kubwa iliyofanywa na Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi katika kutatua shida za wananchi.

Akizungumza katika ziara ya Makamu wa Pili wa Rais Hemed Suleiman Abdulla, eneo la Mpendae, Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar, Idara tikadi, Uenezi na Mafunzo Khamis Mbeto Khamis alisema, OMO kwenye ziara yake badala ya kueleza jinsi Serikali ilivyofanikiwa kutatua shida za wananchi, yeye amebaki kudai mambo yasiyo na msingi.

“Aliomba ruksa kwenda Ungereza, huko hana cha kuwaeleza, mara ooh…tulikubaliana tugawane madaraka, mara kuna watu walikataliwa kuandikishwa daftari la wapiga kura hana cha kusema,” alisema Mbeto.

Aliendelea kusema: “hao ambao hawakuandikishwa wanadhani kuwa na kitambulisho cha Ukaazi ndio kuandikishwa katika daftari la wapigakura, jambo ambalo si kweli.”

Alisema, Sheria ya Uchaguzi Zanzibar, Namba 4 ya Mwaka 2018, Ibara ya 15, kifungu kidogo cha 12 kinaeleza sifa ya anayestahili kuandikishwa.

“Hata yeye OMO, anajua lazima uwe umeishi sehemu husika kwa miezi 36, ndio maana hata yeye alipoenda kujiandikisha Kikwajuni Bosnia, haikuwezekana, Mbweni alipohamia pia hakuwa na sifa, akaja kujiandikisha hapa Mpendae” alisema Mbeto na kumtaka OMO aache kudanganya “anafanya hivyo kwa kuwa hana hoja.”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here