Ni ‘derby’ ya kibabe, hakuna mshindi

0

Na Jumbe Abdallah

BAO la Stephan Aziz KI lililofungwa dakika ya 45 ya kipindi cha kwanza, limetamatisha ‘Kariakoo derby’ kwa sare ya 1-1.

Simba ndio walikuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza dakika ya 15 ya kipindi cha kwanza kupitia kwa Augustine Okrah (Okrah Magic) ambaye alipokea pasi kutoka kwa Clatous Chama (Tripple C, Mwamba wa Lusaka) na kupachika bao hilo.

Mchezo huo wa aina yake ulionekana kuwa na kasi zaidi kipindi cha pili, ambapo kila upande ulipeleka mashambulizi kwa zamu, na hadi dakika ya 90, filimbi la mwamuzi Ramadhani Kayoko ilimaliza ubishi wa nani zaidi kati ya miamba hao wa soka Tanzania na Afrika Mashariki; Simba na Yanga.

Kutokana na sare hiyo, wababe hao wamefungana pointi; kila mmoja ana pointi 14, ingawa Simba wanaendelea kusalia kwenye kilele cha msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here