Mtendaji Mkuu UCSAF afanya ziara ya kutathmini utekelezaji wa miradi ya mawasiliano wilayani Kilolo

0

MTENDAJI Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Mhandisi Peter Mwasalyanda, amefanya ziara ya kikazi wilayani Kilolo, mkoani Iringa, ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry Silaa.

Lengo kuu la ziara hiyo lilikuwa ni kufanya tathmini ya utekelezaji wa miradi ya mawasiliano inayotekelezwa kwa ruzuku ya serikali kupitia UCSAF pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili wananchi hususan walioko vijijini.

Katika sehemu ya awali ya ziara yake, Mhandisi Mwasalyanda alitembelea mnara wa mawasiliano wa kampuni ya Vodacom uliopo katika kijiji cha Ibofwe ambao umejengwa kwa ruzuku ya serikali kupitia UCSAF kwa gharama ya Shilingi Milioni 122.6.

Mnara huo ni miongoni mwa juhudi za serikali kuhakikisha wananchi wa maeneo ya pembezoni wanapata huduma bora za mawasiliano.

Akiwa katika ziara hiyo, Mhandisi Mwasalyanda pia alitembelea Shule ya Sekondari Nyalumbu ambapo alikagua chumba kilichotengwa kwa ajili ya maabara ya kompyuta.

Baada ya kujiridhisha na maandalizi yaliyofanyika shuleni hapo, aliahidi kuwa shule hiyo itaingizwa kwenye mpango wa mwaka huu wa fedha kwa ajili ya kufikishiwa vifaa vya TEHAMA, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuinua elimu ya kidigitali nchini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here