Mradi wa ‘Girls in ICT’ ulivyohamasisha wasichana kuwa wavumbuzi wa Kiditijali

0

SERIKALI kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) imeendelea kuwekeza katika juhudi za kuwahamasisha watoto wa kike kushiriki kikamilifu katika masomo ya STEM (Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati) kupitia mradi wa ‘Girls in ICT.’

Mradi huu unalenga kuwawezesha wasichana kupata ujuzi wa kiteknolojia na kuimarisha uwezo wao wa kiteknolojia, huku wakijiandaa kushiriki katika maendeleo ya kidijitali ya taifa na kufanikisha usawa wa kijinsia katika sekta ya sayansi na teknolojia.

Katika kipindi cha mwaka wa Fedha 2024/25 pekee, mradi huu ulifikia washiriki ambao ni wanafunzi wa kike 246 wa shule za Sekondari za umma kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar.

Kupitia kambi sita za mafunzo ya kikanda zilizofanyika mwezi Aprili mwaka huu, washiriki walijifunza matumizi halisi ya STEM, kuimarisha fikra za kina, kushirikiana katika timu, na kutatua changamoto kwa kutumia mifumo ya Arduino na microcontrolles.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here