NAIBU Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Wanu Hafidh Ameir, amesisitiza urejeshaji wa mikopo ya elimu ya juu kwa kuzingatia uwezo wa kila mnufaika, hususan walioko sekta isiyo rasmi.
Akizungumza Aprili 17, 2026 Jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kampeni ya “Kiduchu”, Wanu amesema kuwa katika kipindi cha miaka mitano, Serikali imetoa TZS 3.6 trilioni kwa wanafunzi wa vyuo, hatua iliyowezesha vijana wengi kupata elimu bila vikwazo vya kifedha.
Ameongeza kuwa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wA Elimu ya Juu ( HESLB) imeimarisha ukusanyaji kupitia uhamasishaji, lakini changamoto bado ipo kwa wanufaika wenye kipato cha chini ambao hawajaanza au wamesitisha urejeshaji.
Akizungumza Kampeni ya “Kiduchu” yenye kaulimbiu “Fresh, Tunasonga!” amesema kuwa inalenga kuwahamasisha wanufaika kuanza kurejesha kuanzia Shilingi 5,000 na kwamba inawalenga wanufaika 135,186 wanaodaiwa jumla ya Shilingi 920 Bilioni.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Prof. Hamisi Dihenga wameeleza kuwa kampeni hii inazingatia hali halisi ya kipato cha wanufaika, ikilenga kuendeleza juhudi Mbalimbali zilizoanzishwa na Bodi za kukusanya Mikopo iliyoiva ikiwemo Kampeni za “Sifurisha”