Mkakati wa kutangaza Utalii Kanda ya Kusini wazinduliwa

0

WAZIRI wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt. Pindi Chana amezindua Mikakati miwili (2) ya Kutangaza Utalii Kanda ya Kusini inayotekelezwa kupitia Mradi wa Kuboresha Usimamizi wa Maliasili na Kukuza Utalii Kusini mwa Tanzania (REGROW) katika hafla iliyofanyika mkoani Njombe.

Balozi Dkt.Pindi Chana amebainisha kuwa katika kufungua utalii mwaka 2017 Serikali ilianzisha Mradi wa Kuboresha Usimamizi wa Maliasili na Kukuza Utalii Kusini mwa Tanzania (REGROW) kwa lengo la kupanua wigo wa mazao ya utalii kijiografia kwa kuendeleza Sekta ya Utalii katika mikoa ya Kusini.

Waziri Balozi Dkt. Chana amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa maono makubwa ya kuibeba sekta ya Utalii nchini si tu kwa Filamu ya ‘The Royal Tour’ bali kupitia miradi na programu mbalimbali za kimkakati ukiwemo REGROW.

Katika uzinduzi huo, Balozi Dkt. Chana ameongeza kuwa Mikakati hiyo miwili imeainisha hatua mbalimbali ziyaakazochukuwa ili kuchochea ukuaji wa shughuli za utalii katika Mikoa ya Kusini ikiwemo Mikoa ya Iringa, Njombe, Ruvuma, Rukwa, Katavi, Mtwara, Lindi, Songwe, Mbeya, na Morogoro.

“Ni matarajio yetu kuwa, utekelezaji wa Mikakati hii utaongeza idadi ya watalii wanaotembelea ukanda huu hivyo kunufaika na faida zitokanazo na shughuli za utalii ikiwemo ongezeko la ajira na fursa za uwekezaji, mapato ya Serikali na mapato ya mwananchi mmoja mmoja,” alisema Waziri Balozi Dkt. Chana

Uzinduzi wa Mikakati hiyo ulioambatana na maonesho ya shughuli za Taasisi za umma na binafsi, umehudhuriwa na Mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao hapa Tanzania, Wakuu wa Mikoa ya Kanda ya Kusini, Taasisi za umma na binafsi, Wadau mbalimbali, Viongozi wa Kisasa, Viongozi wa Dini, Wazee wa Mila, Viongozi mbalimbali na wananchi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here