HADI kufikia Agost 15, 2025, jumla ya minara 661 tayari imekamilika na imeanza kutoa huduma kwa wananchi ikiwa ni sawa na asilimia 87.20 ya utekelezaji wa mradi huu muhimu kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Mradi huu unatekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali kupitia UCSAF na makampuni ya simu ambayo ni Airtel, Halotel, Honora (YAS), TTCL na Vodacom.