Mbunge ACT ‘akunwa’ na utekelezaji miradi wa Rais Dkt. Mwinyi

0

Na Mwandishi Wetu, Dodoma


MBUNGE wa Konde, wilaya Micheweni kwa tiketi ya ACT Wazalendo Mohamed Saidi issa, amesema miradi ya kijamii na uwekezaji jimboni kwake imekuwa mkombozi wao kiuchumi na kijamii.

Akizungumza Jijini Dodoma jana kabla ya kuanza Bunge la 12, mkutano wa 18, kikao cha kumi nne, mbunge huyo alisema, ujenzi wa miundombinu ya kijamii na uwekezaji unaofanywa hivi sasa, umetatua changamoto nyingi zilizokuwa zinawakabili.

Alisema, mambo mengi aliyokuwa anayapigia kelele bungeni hivi sasa yamerekebishwa ikiwa ni pamoja na kuwepo hospitali.

“Kinamama walikuwa wanaona bora kuzalia nyumbani, lakini sio kutoka kwenda Hospitali Micheweni,” alisema.

Alibainisha kuwa, watoto pia walikuwa wakienda shule za mbali, lakini hivi sasa jimboni kwake anazo shule tatu za kisasa.

“Hoteli za kitalii zimejengwa, tunashukuru na changamoto zingine huenda zikatatuliwa, Konde wananchi wanafurahi,” alisema.

Aliendelea kusema, maji yalikuwa shida kwani hata visima walivyochimba kwa nguvu zao wenyewe na pesa za mfuko wa jimbo vilikauka sasa wana maji ya bomba.

Mbunge huyo ameahidi kuwania nafasi hiyo muhula mwingine na akishindwa atakubali matokeo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here