Mbio za magari ndani ya msitu wa ‘Sao Hill’ zafana

0

Na Fredy Mgunda, Iringa

Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt. Pindi Chana amevutiwa na ubunifu na mawazo mazuri yaliyofanywa na Shamba la Serikali Sao hili kwa kuandaa Mashindano ya mbio za Magari katika msitu huo kwani ni fursa kubwa ya kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo kwenye Shamba hilo.

Balozi Dkt. Chana ameyasema hayo wakati akizungumza kwa njia ya simu katika Mashindano Sao Hill Misitu auto Cross Tanzania the Royal Tour kwa kushirikiana Iringa Motorsports club Tanzania kwa ubunifu huo kwani unaumuhimu mkubwa katika masuala mazima ya kutangaza utalii.

“Haya ni maelekezo ya Rais wetu Samia Suluhu Hassan ambaye alituelekeza kuendelea kubuni vyanzo mbalimbali vya utalii kwani ndio chanzo kimoja wapi katika masuala mazima ya utalii wa aina hiyo wa mashindano ya mbio za mahari au Rally katika misitu yetu ambavyo tunaihifadhi mwenye maeneo yetu .” alisema Dkt. Balozi Chana.

Aidha, alieleza Mkakati wa wizara ni kuwa na tukio litakalohusisha masuala ya michezo mbalimbali ambalo litafanyika katika maeneo ya hifadhi za Serikali ikiwemo msitu katika eneo la Sao hill.

“Ni jambo zuri na tuendelee kuratibu ili liweze kufanyika mara kwa mara kadiri Kamati ya maandalizi tutakavyoamua ili kupata washiriki wengi zaidi.” alisema Waziri huyo.

Kwa upande wake Mhifadhi Mkuu wa Shamba la Sao hill Lucas Sabida alisema, wameandaa mashindano mafupi ya mbio za mahari, lakini wana mpango wa kuandaa mashindano makubwa zaidi.

Alisema, lengo la mashindano hayo ni kuendelea kujitangaza kama Shamba la TFS kwa ajili kutangaza utalii wa ikolojia na nyuki kupitia utalii wa michezo wa mbio za Magari kutokana na mwitikio kuwa mkubwa kwao Wananchi.

Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Saad Mtambule alisema, wilaya hiyo ina misitu Msingi, ambapo wana zaidi ya hekta 100,000 ambayo inatumiwa kwa ajili ya uzalishaji wa mbao pamoja na bidhaa zingine kama Marine boad, Mirunda na nguzo za umeme.

Alisema, mazao hayo wamekuwa wakiyatumia na kuwasaidia kwa uchumi na mapato kwa mustakabali wa jamii, lakini kupitia Program ambayo ilianzishwa na Rais wa Jamhuria ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ‘The Royal Tour.’

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here