Mbio kudumisha ushirikiano wa Tanzania na India kufanyika Dar

0

Na Brown Jonas – WUSM

WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Damas Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa India nchini Tanzania, Binaya Pradhan ambapo pamoja na mambo mengine viongozi hao wamejadili kuhusu tukio la mbio za pamoja za kudumisha ushirikiano kati ya Tanzania na India “The Friendship Run between India and Tanzania with Milind Soman” linalotarajia kufanyika jijini Dar es Salaam kati ya Desemba 30 na 31, 2023.

Akizungumza kuhusu tukio hilo hivikaribuni, Ndumbaro alisema Serikali ya India imeomba ushirikiano na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ili kufanikisha tukio hilo ambalo pia litahudhuriwa na mwanariadha maarufu kutoka nchini India Milind Soman.  

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here