Mbeto: Uchaguzi ni mapambano ya ushindani wa sera na hoja, si lelemama

0

Na Mwandishi Wetu, Pemba

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimewataka Viongozi na wanachama wake Kisiwani Pemba kujiandaa kisaikolojia na kujipanga kimkakati tayari kushiriki Uchaguzi Mkuu, Oktoba mwaka huu

Pia, chama hicho kimesema Uchaguzi si jambo dogo, bali ni mapambano ya sera na hoja.

Maelezo hayo yametolewa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis, alipozumgumza na makundi ya viajna Wahamasishaji na Wasanii katika Ukumbi wa Makonyo, Wawi, Pemba.

“Uchaguzi si kama kucheza lelelmama au singeli” alisema Mbeto.

Mbeto alisema, kila kiongozi na wanachama kwa nafasi zao, wanatakiwa kuhahakikisha wanafanya kila linalowezekana ili kupata ushindi wa kidemokrasia kwa kuwahamasisha wanachama na wananchi.

Alisema, matokeo ya ushindi wa uchaguzi ni baada ya chama kutangaza sera zake, wananchi kupiga kura, kuhesabiwa na matokeo kutangazwa.

Alisema, ni matarajio ya kila chama cha siasa kipate idadi kubwa ya kura kwa kuwa uchaguzi si simulizi za hadithi au maneno matupu.

“Chama chenu kinawataka viongozi wote mjipange na kujiandaa kimkakati kuelekea Oktoba Mwaka huu. Uchaguzi umeshapiga hodi hivyo lazima tukumbushane mapema na kuanza kujipanga ” alisema Mbeto.

Alibainisha kuwa, kila unapomalizika uchaguzi mkuu mmoja, CCM hujiandaa kwa uchaguzi mwingine, hivyo aliwataka wanachama kutobweteka na kufanya mambo kwa mazoea.

“Uchaguzi hubadilika kulingana na mazingira husika. Hata malaria ukipima utakuta idadi ya juu au ya chini ya wadudu wake. Uzoefu katika kila uchaguzi una uzoefu na mazingira yake,” alisema Mbeto.

Katibu huyo Mwenezi alisema, hakuna mtu mwenye uwezo wa kufanya kazi bila kuwashirikisha wenzake huku akiwataka viongozi wa CCM kushirikiana na wanachama wao.

“Wasanii jiandaeni kutunga mashairi ya nyimbo nzuri za hamasa na kampeni. Wahamasishaji lazima mpite kila nyumba, kiambo kwa kiambo, Shehia hadi Shehia kuomba kura kwakuwa huo ni wajibu wa kidemokrasia,” alisema.

Alisema, nyimbo zote zitakazotungwa zitahakikiwa mapema na kupasishwa kabla ya kuimbwa, hivyo aliwataka watunzi wa nyimbo hizo kuanza kutunga mashairi yatakayovutia na kuelimisha wananchi kuhusu Uchaguzi Mkuu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here