Mbeto ajitolea kuwatembeza OMO, Jussa kuona kazi za Rais Mwinyi

0

Mwandishi Wetu, Zanzibar


KATIBU Maalum ya NEC Zanzibar, Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis amejitolea kuwa msindikiza watalii ‘Tour Guide’ ili awatembeze viongozi wa ACT Wazalendo, Zanzibar kwenye miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), chini ya Rais Dkt. Hussein Mwinyi.

Akizungumza na wanahabari 18 Juni 2025, Mbeto alisema Mwenyekiti wa ACT, Othman Masoud Othman ‘OMO’ na Makamu wake, Jussa Ismail Ladhu pengine hawaoni kinachofanyika, hivyo yupo tayari kuwatembeza.

Mwenezi Mbeto alisema, Ilani ya chama hicho inayomalizikia ya 2020/2025 ilikuwa na vipaumbele 10 kama ilivyo ya sasa, tahmini inaonyesha imefanya vizuri pande zote mbili.

“Mapinduzi makubwa ya kimaendeleo yamefanyika tangu Rais Dkt. Mwinyi aingie madarakani, jamaa yangu Jussa juzi nimemsikia akidoboha (akibeza) miundomboni ya barabara za Mpendae, akasema pesa nyingi zimekopwa jambo ambalo anadai ni ufujaji” alisema.

Mbeto alisema, Serikali inakopa kwa kuwa ina uwezo wa kulipa na hatua hiyo imetokana na kuamua pesa iliyokuwa inatumika kila mwaka kumwaga vifusi ikusanywe kisha wakope kujenga barabara za kudumu.

“Jussa nimuelimishe kuwa, mikopo ya barabara zinazojengwa zinalipwa na pesa za Mfuko wa Barabara ambapo Shilingi 100 inakatwa katika kila lita moja ya mafuta inayouzwa Zanzibar,”

“Zanzibar tunauza wastani wa lita za mafuta Milioni 15 kwa mwezi kuanzia kwenye magari, boda boda hadi ndege achilia mbali ada za leseni za vyombo vya moto,” alisema Mbeto na kuongeza kuwa, hakuna anayebebeshwa deni la mikopo ya barabara kama anavvyodai Jussa.

Mbeto alibainisha kuwa, SMZ ina pesa nyingi kupitia vyanzo hivyo kuliko deni lenyewe na kinachofanyika ni akili kubwa za Dkt. Mwinyi badala ya kuziba ziba viraka kila mwaka bora kukopa na kujenga baada ya kukusanya mapato yatokanayo na mfuko wa barabara.

Zanzibar mtandao yenye Kilomita 1,480, Ilani ilimtaka Rais Mwinyi, ajenge Kilomita 196 lakini kajenga Kilomita 1000 maana yake Ilani imevukwa kwa asilimia zaidi ya 100.

Mbeto alisema, Marekani deni lote duniani wanadaiwa asilimia 35 ya madeni ya nchi zote ulimwenguni, lakini Tanzania haifiki hata asilimia 2 lakini na wanachukua mikopo kuimarisha miundombinu “Jussa na Mwenyekiti wake, wanaposema hiki kibaya, basi waonyeshe kizuri na sio kuropoka.”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here