Mafunzo ya ukusanyaji kodi za majengo kwa mfumo wa Tausi yafanyika Kibaha DC

0

HALMASHAURI ya Wilaya ya Kibaha imeendesha mafunzo ya ukusanyaji wa kodi ya majengo kwa kutumia mfumo wa kielektroniki wa TAUSI, yenye lengo la kuongeza ufanisi wa makusanyo ya mapato ya Serikali za Mitaa.

Mafunzo hayo ya siku mbili yamefunguliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, BRegina Bieda, na yanawahusisha Watendaji wa Kata, Maafisa Mapato, Wahasibu Idara ya Fedha Kwa ujumla pamoja na Maafisa Ardhi.

Akizungumza wakati wa ufunguzi, Bieda amewataka washiriki kushirikiana kwa karibu katika kutekeleza jukumu la ukusanyaji wa kodi ya majengo, akisisitiza kuwa ushirikiano huo ni muhimu katika kukuza mapato ya Halmashauri na Serikali kwa ujumla.

“Mfumo wa TAUSI ni nyenzo muhimu ya kisasa ambayo itarahisisha kazi yenu ya kila siku. Ni wajibu wenu kujifunza, kuelewa na kuutumia ipasavyo kwa kuwa ninyi ndio watekelezaji wakuu katika ngazi ya Kata,” alisema Bieda.

Mafunzo hayo yanaendeshwa na Afisa TEHAMA wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha, Menard Mrimbile, kwa ushirikiano na Maafisa Mapato kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Amiri Madega na Vincent Mirambo.

Wawezeshaji wa mafunzo hayo wamesisitiza umuhimu wa kuelewa kwa kina matumizi sahihi ya mfumo wa TAUSI ili kuhakikisha ukusanyaji wa kodi unafanyika kwa uwazi, ufanisi na uwajibikaji wa hali ya juu.

Mafunzo hayo yataendele kesho ambapo washiriki wataendelea kupata fursa ya kujifunza Kwa vitendo ili kuleta ufanisi katika utekelezaji wake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here