Maelfu wamsindikiza Dkt. Mwinyi kuchukua fomu ya urais

0

Na Mwandishi Wetu

MAELFU ya wananchi wamejitokeza huku mvua ikinyesha kumsindikiza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi, kuchukua fomu ya kuwania Urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika, Oktoba mwaka huu.

Dkt. Mwinyi ambaye aliambatana na mkewe Mariam Mwinyi, alikabidhiwa fomu na kusomewa mambo ambayo anapaswa ayatekeleze ikiwa ni pamoja na kusaka wadhamini 200 katika mikoa mitano ya Zanzibar kisha kurudisha fomu hiyo, kabla ya Septemba 10, mwaka huu.

Mara baada ya kuchukua fomu, msafara wa mgombea huyo, anayetarajiwa kupeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi huo, ulipita mitaa mbalimbali ya Zanzibar ambako wananchi kadhaa walijipanga barabarani na kwenda kuzuru kaburi la Rais wa Kwanza Sheikh Abeid Amani Karume lililopo Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui.

Akiwa Ofisi Kuu Kisiwandui, mgombea huyo alizungumza na wazee wa chama hicho kisha kuelekea viwanja vya Mao Tse Tung ambako atazungumza na wananchi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here