Madiwani Kibaha DC watakiwa kuhamasisha uandikishaji wapiga kura

0

MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha, Regina Bieda, amewataka Madiwani kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye Daftari la Wapiga Kura, ikiwa ni maandalizi ya uchaguzi ujao.

Zoezi hilo linatarajiwa kuanza Februari 13 hadi 19 mwaka huu na walengwa wakuu ni waliofikisha umri wa miaka 18, wale waliohama makazi, pamoja na waliopoteza au kuharibikiwa na vitambulisho vyao vya kupigia kura.

Bieda alitoa wito huo leo, Februari 6, wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo ambapo alisema, ni muhimu kwa Madiwani kuhakikisha wananchi wanajitokeza kwa wingi kujiandikisha.

Aidha, Bieda alizungumzia hali ya ufaulu wa wanafunzi wa elimu ya msingi katika Halmashauri hiyo, akibainisha kuwa matarajio ni kupata matokeo mazuri zaidi mwaka huu.

Alisema, mwaka uliopita, Halmashauri ya Kibaha ilishika nafasi ya tatu kimkoa, na lengo kwa mwaka huu ni kupanda zaidi katika msimamo huo.

“Tunajipanga kuhakikisha tunaendelea kuinua viwango vya elimu kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia,” alisema Bieda.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here