Madereva wa Bajaji Arusha wapewa utaratibu wa kufanya shughuli zao

0

Na Abel Paul wa Jeshi la Polisi

UONGOZI wa wilaya ya Arusha umewataka waendesha bajaji kufuata utaratibu na kuweka mipango mathubuti wa uendeshaji wa shughuli zao katika jiji la Arusha, ambapo wametakiwa kujisajili na kuweka uongozi imara ili kuondoa dhana ya kuwa kundi hilo ni la watu wasio jitambua.

Akifungua kikao hicho kilicho hudhuriwa na bajaji 700, Mkuu wa Wilaya ya Arusha Said Mtanda ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya Arusha amebanisha kuwa, Serikali ina mipango ya dhabiti na waendesha bajaji, ambapo amewataka kuchagua viongozi imara na kufuata taratibu zilizopo ili kutokinzana na Serikali.

Mtanda alibainisha kuwa, kuanzia Oktoba 15, 2022 Serikali katika halamashauri ya jiji la Arusha imesitisha utoaji wa leseni mpya za LATRA ndani ya jiji la Arusha, ambapo amebainisha kwa sasa wameanza kusajili maeneo rasmi ambayo madereva hao watafanya shughuli zao.

Kwa upande wake Mkuu wa Kikosi cha usalama Barabarani Mkoa wa Arusha Mrakibu wa Polisi SP-Solomon Mwangamilo alisema, Jeshi la Polisi kupitia kikosi cha usalama barabarani kimepokea maelekezo ya Serikali katika kusimamia mikakati mipya ya kuboresha na kusimamia waendesha bajaji katika jiji la Arusha.

Nae Kaimu Mkurungenzi wa Jiji la Arusha Hargeney Chitukuro alisema, halmashauri ya jiji la Arusha hawana ugomvi na waendesha bajaji, ambapo amewataka kufuata sheria na taratibu zilizowekwa.

Kwa pande wake Afisa LATRA Mkoa wa Arusha Amani Mwakalebela alisema, wataendelea kutoa Elimu ikiwa ni Pamoja na kuchukua hatua kwa madereva wote watakao kiuka sheria na taratibu za usalama barabarani katika Mkoa wa Arusha.

Akizungumza kwenye kikao hicho, Mwanasheria wa halmashauri ya jiji la Arusha Idd Ndabona alisema, sheria za halmashauri ya jiji la Arusha ziko wazi kwa waendesha bajaji, ambapo amebainisha wao wanashirikina na LATRA katika kutoa dira na kusimamia ikiwa ni Pamoja na kusajili vyombo hivyo.

Nao baadhi ya waendesha bajaji katika jiji la Arusha wameshukuru Serikali kwa kuwapa dira sahihi katika kazi zao za kila siku nakuomba Serikali kusimamia jambo hilo

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here