Kongamano la Klabu za uzalendo lafanyika Kibaha DC

0

HALMASHAURI ya Wilaya ya Kibaha imefanya Kongamano la klabu ya Uzalendo katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Ruvu na Shule ya Sekondari Kilangalanga.

Kongamano hilo limefanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Ruvu na Viwanja vya Shule ya Sekondari Kilangalanga kwa nyakati tofauti.

Akizungumza katika Kongamano hilo Pudenciana Domel ambaye ni Mratibu shughuli hiyo amewaasa Vijana kuwa wazalendo Kwa Taifa lao.

Domel alisema ni wakati wa kila Kijana kujifunza uzaleondo na maadili mema kuanzia ngazi ya Familia hadi sehemu za kazi.

Kwa Upande wake John Pili Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji Mdogo Mlandizi amewataka Vijana kujifunza Uzalendo kupitia Mwenge wa Uhuru Kwani unahimiza uzalendo Kwa Taifa.

Naye Restuta Maira Afisa Ustawi wa Jamii amewataka Vijana hasa wanafunzi kuibua na kuripoti masuala ya ukatili wa kijinsia ili kulinda utu na Maadili.

Furaha Mushi na Abdul Juma ni miongoni mwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya wasichana Ruvu na Kilangalanga kwa nyakati tofauti wameahidi kuwa wazalendo na kutekeleza Elimu iliyotolewa Kwa vitendo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here