Kituo cha RWAMGASA chaongeza thamani ya Kampuni ya wachimbaji wadogo Geita

0

Na Mwandishi Wetu

IMEELEZWA kuwa kutokana na huduma inayotolewa na Kituo cha mfano cha uchenjuaji wa dhahabu kinachomilikiwa na Shirika la Madini la Tanzania STAMICO cha Rwamgasa kimerahisisha na kuongeza thamani ya Kampuni wachimbaji wadogo inayojishughulisha na  uchimbaji wa Madini.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Hexad inayojishughulisha na uchimbaji wa Madini Fortnatus Luhemeja wakati akizungumza katika Kituo cha mfano cha uchenjuaji wa dhahabu kinachomilikiwa na  STAMICO katika kijiji cha Rwamgasa mkoani Geita.

Alisema, kituo hicho kimeongeza thamani kubwa kwenye shughuli zake za uchimbaji wa madini kutokana na kutoa huduma ya CIP ambapo imesaidia kupeleka mawe yao kwa muda mfupi na kuweza kupatiwa dhahabu kutoka kwenye mawe hayo.

Luhemeja alisema, awali walikuwa wakitumia mfumo wa mekiuri ilikuwa inachukua asilimia 25 kwa mekiuri na Vatilishin ilikuwa inachukua 75 hivyo kituo hicho kinachukua asilimia 95 mpaka 97 jambo ambalo limewahakikisha upatikanaji wa dhahabu kwa urahisi.

Aidha, aliongeza eneo hilo limekuwa na historia ya kutumika kabla hata ya uhuru hivyo mpaka sasa wamechimba mpaka mita 76 wakiitafuta dhahabu jambo ambalo inawapa tija na mafanikio.

Kwa kawaida tunaweza kupata Dhahabu toka kwenye mawe yenye Dhahabu kwa kutumia mercury ni 25% tu, tukitumia technology ya VAT Leaching ni 75% tu, ila tunapotumia mfumo wa CIP tunapata 95% hadi 97%.,” alisema Fortunatus Luhemeja.

Aidha, akizungumzia kuhusiana na Shirika la STAMICO alisema, linawasaidia wachimbaji wadogo kwa kuwapatia mafunzo ya mfano ya mara kwa mara ili kurahisisha shughuli zao.

Alisema, kupitia maonyesho ya Madini yanayoendelea STAMICO inawaonyesha namna ambavyo teknolojia inatumika katika masuala ya uchimbaji wa madini.

STAMICO imeendelea kuwa mlezi wa wachimbaji wadogo ili hatimaye waweze kukua na kuongeza tija katika kufanya shughuli zao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here