RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewataka viongozi wa dini, wanasiasa, waandishi wa habari na wananchi kwa ujumla kukemea kauli zinazoweza kuvuruga amani, hususan kuelekea uchaguzi mkuu.
Akizungumza katika Baraza la Maulid lililofanyika Ukumbi wa Chuo cha Polisi Ziwani, Dkt. Mwinyi alisema, hakuna taifa linaloweza kuendelea bila amani ya kudumu na kuwataka wanasiasa kuepuka siasa za chuki na mifarakano.
Aidha, aliwahimiza waumini wa Kiislamu kufuata mafunzo ya dini yao ili kudumisha mshikamano, huku akisisitiza kuwa “Amani na Utulivu ni Tunu.”