Jafo: Mita zote za umeme lazima zifikishwe Wakala wa Vipimo

0
WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Dkt. Selemani Jafo

WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Dkt. Selemani Jafo ameagiza Mita zote za Umeme zipelekwe Wakala wa Vipimo (WMA) ili kupima ubora wake kabla ya kufungiwa wananchi.

Jafo alitoa maagizo hayo jijini Dodoma alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Wakala huo, lililopo eneo la Medeli, ambapo alisema, ukaguzi huo utasaidia kuwapunguzia wananchi gharama kwa kulipa bili zisizostahili.

“Naelekeza mita zote za umeme lazima zifikishwe Wakala wa Vipimo (WMA) ili kuzipima kwa lengo la kuwapunguzia gharama wananchi, lengo ni kuepusha wananchi kufungiwa mita ambazo hazina ubora na mwisho wa siku wakalipa bili zisizostahili,” alisema Jafo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here