Hakuna chama cha kuiondoa CCM madarakani-AAFP

0

Mwandishi Wetu

MGOMBEA Urais Zanzibar kupitia Chama cha Wakulima (AAFP), Said Soud amesema, hakuna chama cha siasa kinachoweza kuiondoa CCM madarakani bila vyama kuungana.

Akizungumza wakati akitangaza kupeperusha bendera ya chama hicho ngazi ya Urais katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu, Soud alisema tatizo kila mmoja anataka awe Rais.

“Kila mmoja anataka mgombea awe yeye, ajionyeshe yeye kuwa ndio mwenye uwezo, itawezekana vipi?” alihoji.

Alisema, miezi sita iliyopita aliwahimiza na kuvitaka vyama kuunganisha nguvu ili kuweza kukitoa CCM madarakani, lakini hakuna chama kilichojitokeza, ndio maana yeye na chama chake wameamua kupambana wenyewe.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here