‘Fuatilieni afya zenu kama mnavyofuatilia mpira’

0
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya Dkt. Festo Dugange.

Na Hytham Iddy

NAIBU Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya Dkt. Festo Dugange amewakumbusha wananume kufuatilia afya zao na Afya za Watoto kama wanavyofuatilia mechi za mataifa ya Africa AFCON2023 yanayoendelea nchini Ivory Coast na Tanzania imeshuka dimbani kucheza mechi ya kwanza ya mashindano hayo dhidi ya Morocco iliyoshinda goli 3 kwa sufuri.

Dkt. Dugange ameitoa kauli hiyo katika uwanja wa Mbagala Zakhem mkoani Dar Es Salaam wakati akizundua zoezi la uchunguzi wa Afya na Chanjo kwa wananchi wa mkoa huo zoezi lilillowakutanisha wananchi kutazama mechi hiyo kwenye ‘Big Screen’ iliyofungwa katika uwanja huo kwa ajili ya hamasa kwa timu ya Taifa.

“Tuna mwamko mkubwa katika kufuatilia michezo hususani AFCON2023 tunapenda sasa mwamko huo akinababa wenzangu kujali na kulinda afya kinga kwa Watoto maana akinamama wametuzidi mbali juu ya Afya ya Watoto wetu na kuzingatia Afya zao wenyewe,” Dkt. Festo Dugange

Zoezi hilo linaloendelea katika viwanja hivyo limeratibiwa na Shirika la Johs Hopkins University (JHU) kupitia mradi wa Breakthrough ACTION unaofadhiliwa na USAID kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI na Wizara ya Afya.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here