DNA yamuweka huru aliyefungwa miaka 38 kimakosa

0

CALIFONIA, Marekani

RAIA mmoja wa Marekani mwenye asili ya Afrika ameachiwa huru baada ya kufungwa jela kwa karibu miongo minne kwa kosa ambalo hakulifanya.

Maurice Hastings, aliachiwa huru katika jimbo la California, baada ya vipimo vya msimbojeni (DNA) kuonesha kuwa hakuhusika na kosa la mauaji aliyodaiwa kufanya.

Ofisi ya Mwanasheria wa Los Angeles imemuachia huru Hastings, na kukiri kuwa, alihukumiwa na kufungwa kimakosa, kwa madai ya kumteka nyara na kumuua Roberta Wydermyer, katika jiji la Inglewood mwaka 1983.

Vipimo vipya vya vinasaba (DNA) vimemuondoa hatiani raia huyo mweusi wa Marekani, na kutambua mtu mwingine kuwa mhusika wa mauaji hayo.

Hata hivyo, inaelezwa mhusika halisi wa mauaji hayo ya mwaka 1983 alifia gerezani mwaka 2020, akitumikia kifungo cha mashitaka tofauti ya utekaji nyara na ubakaji.

Mwanasheria wa Los Angeles, George Gascon licha ya kumuomba radhi Hastings kwa kufungwa miaka 38 kimakosa, amekiri kuwepo mapungufu katika mfumo wa mahakama wa Marekani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here