RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewahimiza Wananchi kuendelea kuiombea nchi amani Ili Maendeleo zaidi yapatikane.
Alhaji Dkt. Mwinyi ameyasema hayo alipojumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika Sala ya Ijumaa Msikiti wa Weles Kikwajuni Wilaya ya Mjini.
Alhaji Dkt, Mwinyi amewasisitiza Waumini na Wananchi kuweka Azma ya Kuendeleza Amani iliopo hususani wakati huu wa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Mwezi Oktoba.
Amefahamisha kuwa kipindi cha Miaka mitano ya Awamu ya Nane Mambo mengi ya Maendeleo yamefanyika katika Nyanja zote kutokana na Nchi kuwa na Amani hivyo kuna Wajibu wa kudumishwa.
Aidha, Alhaji Dkt , Mwinyi amewanasihi Waumini hao Kuongeza bidii katika Ibada katika kumi la Mwisho la Mwezi wa Ramadhani.