RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ametunukiwa Shahada ya Heshima ya Uzamivu (PhD Honoris Causa) ya Uchumi iliyotolewa na Chuo Kikuu cha Zanzibar (ZU), ambayo ilitangazwa rasmi Desemba 2024 katika mahafali ya Chuo hicho.
Mkuu wa Chuo hicho, Mhandisi Abdulqadir Othman Hafez, alikabidhi rasmi Shahada hiyo kwa Rais Dkt. Mwinyi Ikulu Zanzibar Agosti 25, 2025.
Aidha, Rais Dkt. Mwinyi amekipongeza Chuo hicho kwa kuthamini na kutambua juhudi zake katika kukuza uchumi na kuleta maendeleo ya Zanzibar, hatua ambayo ameieleza kuwa itamwongezea ari ya kuendeleza maendeleo zaidi nchini.