Dkt. Mwinyi aahidi kuendeleza kasi ya maendeleo

0

MGOMBEA Urais wa Zanzibar kupitia CCM, Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Septemba 13, 2025 amezindua rasmi kampeni za Chama Cha Mapinduzi katika Uwanja wa Mnazi Mmoja, Mjini Magharibi.

Ameahidi kuendeleza kasi ya maendeleo endapo atachaguliwa tena, akisisitiza amani na mshikamano kuwa msingi wa maendeleo.

Vipaumbele vyake ni pamoja na:
✅ Elimu na Afya
✅ Kilimo na Viwanda
✅ Ujenzi wa miundombinu
✅ Ajira kwa vijana (zaidi ya 350,000)
✅ Mikopo na uwezeshaji wananchi
✅ Nyumba za makaazi na hifadhi ya jamii

Halikadhalika, Dkt. Mwinyi amesema uchumi wa Zanzibar umekua kwa 7.4%, na Serikali ijayo inalenga kuongeza kasi hiyo kupitia uwekezaji, utalii na viwanda.

Amesisitiza kampeni za CCM zitakuwa za kistaarabu na kuhubiri amani, huku akiomba wananchi waendelee kukiamini chama hicho na kuwachagua wagombea wake wote pamoja na Dkt. Samia Suluhu Hassan.

r

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here