Waziri Mkuu, Dkt Mwigulu Nchemba akikagua maendeleo ya ujenzi wa Bwawa la Maji la Kidunda mkoani Morogoro, Januari 2, 2026. Wa tatu kulia ni Waziri wa Maji, Jumaa Aweso na kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa mazingira Dar es salaam (DAWASA), Mhandishi Mkama Bwire. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
WAZIRI Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba leo Januari 02, 2026 amezungumza na wakazi wa Tindiga wilaya ya kilosa mkoani Morogoro ambao wameathirika na mvua zinazoendelea kunyesha nchini.
Dkt. Mwigulu amewaeleza wakazi hao kuwa Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan ilishaanza mikakati ya kukabiliana na athari za mvua katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa morogoro kwa kutekeleza mradi wa ujenzi wa Mabwawa eneo la Kidete.
Amesema kuwa ujenzi wa mabwawa hayo ya maji yatakuwa ni suluhisho la kudumu ya mafuriko katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Morogoro.
Ameongeza kuwa kwa sasa mpango huo upo katika hatua za kitalaam ikiwemo kumpata mkandarasi. ”Fedha imepatikana kwa ajili ya ujenzi wa mabwawa kwa sasa tunaendelea na taratibu za kitaalam, Wizara zinazohusika hakikisheni mnakamilisha taratibu hizo ili ujenzi uanze”