π ππ±πͺπ¨πͺπ’ π€π©π’π±πΆπ° πΆπ΅π¦π¬π¦ππ¦π»π’π«πͺ πΈπ’ ππππ 2050
WAZIRI Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba amesema bado kuna fursa nyingi za ushirikiano wa kiuchumi baina ya Taifa la Qatar na Tanzania ambazo zikitumiwa vizuri zitawanufaisha raia wa nchi zote mbili.
βBado tuna fursa nyingi ambazo tunaweza tukanufaika nazo kama tutatekeleza baadhi ya shughuli za kiuzalishaji. Tanzania kama lango la Afrika Mashariki, Kusini na Kati na Qatar kama lango la Mashariki ya Kati na Umoja wa Nchi za Ghuba tulikubaliana kuwa tukichangamkia fursa zote zinazojitokeza, tutaongeza ushiriki wa wananchi wa nchi zote mbili,β alisema.
Alikuwa akizungumza na Rais na Mtendaji Mkuu wa Power International Holding (PIH), Ramez Al-Khayyat na baadhi ya viongozi wakuu wa taasisi hiyo kwenye makao makuu ya kampuni hiyo yaliyopo Lusail, jijini Doha.
Waziri Mkuu alimshukuru Rais na Mtendaji Mkuu wa PIH kwa kuonesha nia ya dhati ya kuwekeza katika sekta ambazo DIRA 2050 imeyaainisha kama maeneo ya kipaumbele.
βTunashukuru kwamba hii kampuni imeonesha nia ya kuwekeza kwenye maeneo yaliyotajwa katika DIRA 2050 ambayo na sisi tumeyawekea kipaumbele. Wameonesha nia ya kushiriki DIRA yetu kupitia utekelezaji wa fursa zilizopo. Tumekubaliana kwamba mawaziri waliopo wakiongozwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Mheshimiwa Kapinga wafuatilie kwa karibu ili utekelezaji uanze mara moja.β
Kwa upande wake, Rais na Mtendaji Mkuu wa PIH, Ramez Al-Khayyat alimweleza Waziri Mkuu kwamba Power International Holding ni kampuni kubwa ya kimataifa inayomilikiwa na watu binafsi ambayo inaendesha kampuni tanzu 400 zenye wafanyakazi 65,000 katika nchi 26.
Kati ya nchi 26, za Afrika ni Misri, Libya, Morocco, Algeria, Mauritania na Rwanda. Alisema wameshaingia makubaliano na Ethiopia (ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa) na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (ujenzi wa barabara yenye urefu wa KM. 400).