OR -TAMISEMI
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Angellah Kairuki amesema Serikali kupitia miradi ya kupendezesha miji (TACTIC), itapeleka Shilingi Bilioni 9.45 katika bajeti ya mwaka wa fedha wa 2023/24 kwa ajili kutekeleza miradi ya maendeleo katika halmashauri ya wilaya ya Kasulu Mji mkoani Kigoma.
Waziri Kairuki alisema katika Mkutano wa hadhara wa Rais Samia Suluhu Hassan na wananchi wa Kasulu Mjini Mkoa wa Kigoma katika ziara yake ya kikazi mkoani humo.
Alisema, Shilingi Bilioni 3.45 itaelekezwa katika Ujenzi wa kituo kipya cha mabasi Murusi katika halmashauri ya wilaya ya Kasulu Mji.
Waziri Kairuki ameeleza, kiasi cha Shilingi Bilioni 2.3 zitatumika kukarabati soko la Kumsenga na Shilingi Bilioni 3.7 zitaelekezwa kwenye Ujenzi wa barabara yenye urefu wa Kilometa 3.2 kwa kiwango cha lami katika mji wa kasulu.
Aidha, Waziri Kairuki alisema katika bajeti ya mwaka wa fedha wa 2022/23, Halmashauri ya Mji wa Kasulu ilipatiwa Shilingi Bilioni 2.4 kwa ajili ya kutengeneza barabara kupitia TARURA.
Vile vile, Waziri Kairuki ameeleza kuwa halmashauri ya wilaya ya Kasulu ilipatiwa kiasi cha Shilingi Bilioni 2.2 kufungua mitandao ya barabara kupitia TARURA.