Na Mwandishi Wetu
ALOYCE Tendewa kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) jina lake limepitishwa kwenda kwa wajumbe kuwania nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Kilombero, Mkoani Morogoro.
Kada huyo ambaye aliwahi kuwa Msaidizi wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Marehemu Edwald Lowasa, jina lake limo kati ya majina nane yaliyopitishwa na Kamati Kuu ya CCM na kutangazwa na Katibu wa Uenezi, Itikadi na Mafunzo CPA Amos Makala.
Tendewa ni mmoja wa wagombea wachache ambaye anaishi Jimboni humo tofauti na wengi ambao wanaishi nje ya Jimbo la Kilombero.