Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
WABUNGE, Wawakilishi na Madiwani wa CCM walichopanda kipindi wamepewa dhamana na chama na wananchi ndicho watakachovuna kuelekea Uchaguzi Mkuu, Oktoba 2025.
Akizungumza katika Mkutano wa Umoja wa Wanawake (UWT) wa chama, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar, Idara Itikadi, Uenezi na Mafunzo Mbeto Khamis Mbeto alisema uwajibikaji na uaminifu ndio kitakuwa kigezo.
Mbeto alisema, wakati utakapofika wa chama kupitisha majina ya wabunge, wawakilishi na madiwani kitakachoangaliwa katikanngazi ya uteuzi ni uwajibikaji wa mtu na uaminifu wake na sio vingine.
Alisema, CCM ni chama cha kuwatumikia wananchi tena zaidi wale wanyonge, hivyo aliyepewa dhamana na atapimwa kwa vigezo hivyo na husika.
Katika mkutano huo ambao Mbunge wa Viti Maalum Tawheeda Galus alimpongeza katibu wake kwa kuwajibika ipasavyo kipindi anachokuwa bungeni, Mbeto alisema UWT ni nguzo muhimu ktk chama hicho.
“Ipo wazi, ukitaka jambo lifanikiwe mkabidhi mwanamke,” alisema.
Alibainisha kuwa mfano ni jinsi jumuia hiyo ilivyofanikisha wanachama wengi wa CCM walivyojitokeza kujiaandikisha ktk daftari la wapiga kura.
“Mlianzia Pemba na daftari, likaja Unguja na sasa tunasubiri kampeni, upigaji kura na kushangilia ushindi” alisema.
Alibainisha pia kuwa hata mambo makubwa yanayofanywa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan yanaonyesha uwezo mkubwa walio nao wanawake.
Mbeto alisifu utendaji wa mbunge huyo viti maalum ambaye alisema kuwa mkoa huo una majimbo 10 na kote amewajibika.
“Majimbo yote 10 umegusa, napendaa kukupongeza” alisema.
Mbeto amewaonya watia nia kuwa wasubiri Bunge livunjwe na chama kitangaze na sio kupita majimboni kipindi hiki kwani bado wenyewe wapo katika majimbo yao.