Mariam Mwinyi atoa sadaka ya Eid kwa vituo vya watoto Z’bar

0

MKE wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF), Mama Mariam Mwinyi amewasisitiza watoto kuendelea kuwa na tabia njema baada ya kumaliza Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Mariam Mwinyi amesema hayo alipovitembelea Vituo vya Watoto ikiwemo cha kituo cha SOS, Mazizini na Zaso Fuoni Mambosasa kwa kuwapatia zawadi mbalimbali ikiwemo mabegi ya shule katika Mkoa wa Mjini Magharibi Machi 31, 2025.

Aidha, Mariam Mwinyi ameviomba vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha wanaimaimarisha usalama katika sehemu zote ambazo kutakuwepo michezo ya kufurahishiha watoto katika kipindi hichi cha Sikukuu ya Eid El Fitr .

Halikadhalika, Mariam Mwinyi amewataka Walezi na Wazazi kuwa waangalifu na Watoto kwa kuzingatia alama za usalama barabarani kipindi hichi cha Sikukuu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here