RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewasisitiza Waumini wa Dini ya Kiislamu kuendelea kuiombea Nchi Amani wakati huu ikielekea katika Uchaguzi Mkuu pamoja na Viongozi Wakuu wa Nchi .
Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo alipozungumza na Waumini wa Dini ya Kiislamu baada ya Kujumuika katika Sala ya Ijumaa, Msikiti wa Ijumaa Mpapa Mkoa wa Kusini Unguja Machi 14, 2025.

Amefahamisha kuwa Maendeleo yanayofikiwa hivi sasa hapa nchini yanatokana na kuwepo kwa Amani na kuahidi kuendeleza Juhudi za kuleta Maendeleo Zaidi.
Aidha, Rais Dkt.Mwinyi amewahakikishia Wananchi wa Mpapa kuwa Serikali itazifanyia Kazi Changamoto za Kijamii ziliomo katika kijiji hicho.

Changamoto hizo zilizobainishwa na Wananchi ni Uchakavu wa Barabara za ndani, Ukosefu wa Uzio katika Skuli ya Mpapa na Ukosefu wa huduma za Karibu za Afya kutokana na kutomalizika kwa Kituo cha Afya kiliopo kwa Miaka mingi ambacho kimejengwa kwa nguvu za Wananchi.
Vilevile, Rais Dkt. Mwinyi amewahakikishia kuwa Serikali itamaliza Changamoto hizo alizoziielezea kuwa ni za Muhimu.
