RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema Zanzibar inafanya kila juhudi kuhakikisha inaongeza idadi ya Watalii kutoka Barani Asia.
Dkt.Mwinyi alisema hayo alipozungumza na Waigizaji na Watengenezaji wa Filamu kutoka India Waliofika Ikulu Zanzibar Machi 1, 2025.
Aidha, Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa Zanzibar iko tayari kushirikiana na India kutangaza Vivutio vya Utalii nchini humo na kuwataka kuwa Mabalozi Wazuri watakapokuwa nchini kwao.
Halikadhalika, Rais Dkt.Mwinyi alisema uzoefu na umahiri wa waigizaji na watengezaji wa Filamu wa India ni fursa muhimu inayoweza kutumika kuitangaza Zanzibar ili kuongeza Watalii kutoka India.
Vilevile, Rais Dkt.Mwinyi amewapongeza kwa kuja nchini na Serikali ipo tayari kushirikiana nao kikamilifu kuitangaza Sekta ya Utalii ya Zanzibar.
Naye, Mkuu wa timu hiyo ya Waigizaji kutoka Taasisi ya JIO CREATIVE LABS Aditya Bhat alisema ziara yao imefungua fursa za ushirikiano na wako tayari kuvitangaza Vivutio vyà Utalii vya Zanzibar nchini India kupitia fani zao.