Mwenyekiti mpya DCPC ahimiza nidhamu

0

MWENYEKITI mpya wa chama cha Waandishi wa Habari Dar es Salaam (Dar es Salaam City Press Club – DCPC), Bakari Kimwanga amesema anahitaji kuona mabadiliko mbalimbali kwenye chama hicho likiwemo suala la nidhamu.

Kimwanga alisema hayo baada ya kuchaguliwa, kwenye uchaguzi uliofanyika leo Februari 28, 2025 kwenye ukumbi wa mikutano wa Anatouglo, jijini Dar es Salaam na kusisitiza, “nidhamu ndiyo msingi wa maendeleo.”

Awali, Mwenyekiti wa Kamati huru ya uchaguzi Wakili wa kujitegemea, Raphael Awino, alimtangaza Kimwaga kuwa Mwenyekiti mpya wa DCPC kwa kupata kura 68 za ndio, na kura nane za hapana na tano ziliharibika.

Kwa upande wa Makamu Mwenyekiti, Mary Geoffrey, amepata kura 70 za ndiyo na saba za hapana na nne zimeharibika.

Aidha, viongozi wengine waliochaguliwa ni wajumbe watano ambao ni Selemani Jongo (69), Penina Malundo (62), Andrew Msechu (67), Khamis Miraji (59) na Veronika Mrema (69).

Uchaguzi huo umefanyika kwa Amani na utulivu, jambo ambalo Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi Raphael Awino amelisifu kuwa la mfano.

Naye, Katibu wa Tume Huru ya uchaguzi, Janet Jovin amepongeza kwa jinsi uchaguzi ulivyofanyika kwa Amani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here