TANAPA yanadi vivutio vyake nchini India

0

SHIRIKA la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) linashiriki Maonesho ya Utalii ya (Outbound Travel Market) OTM 2025 kwa lengo la kunadi vivutio vyake vilivyopo ndani ya Hifadhi za Taifa 21 zinazopatika nchini Tanzania.

Licha ya kutangaza vivutio hivyo pia TANAPA itajikita kuelezea fursa za uwekezaji zilizomo ndani ya hifadhi hizo na kuwahamasisha wawekezaji kuja kuwekeza katika malaza, mazao ya utalii na katika sekta ya usafirishaji ambazo ni injini katika kukuza sekta ya utalii.

Maonesho hayo yanayowakutanisha pia mawakala wa usafirishaji wa ndege kutoka Marekani, Ulaya na Asia yameanza jana Januari 30, 2025 na yanatarajiwa kuhitimishwa Februari Mosi, 2025 huku kwa upande wa TANAPA ikiwakilishwa na Maafisa Utalii kutoka Makao Makuu ya Shirika na Hifadhi za Taifa Kilimanjaro na Mikumi.

TANAPA inatambua kuwa India ni soko linalokua kwa kasi katika utalii wa Kimataifa kutokana na wingi wake wa watu na inaendelea kuchipukia katika teknolojia. Kwa kutambua hivyo TANAPA imeona ni vyema kutumia nafasi hii ya maonesho kutangaza vivutio vyake.

Sambamba na maonesho hayo picturea, TANAPA imeandaa kampeni ya kutangaza vivutio vyake kupitia “Roadshow” katika miji ya Delhi, Chennai, na Bengaluru. Vilevile, TANAPA imepanga kukutana na mawakala wa utalii na usafirishaji ili kukuza na kuendeleza ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na India.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here