Makalla ampongeza Dkt. Mwinyi kwa utekelezaji wa ilani ya CCM

0

KATIBU wa Itikadi na Uenezi CCM Taifa CPA Amos Gabriel Makala amesema, Maendeleo makubwa yanayonekana katika Sekta ya Elimu yanatokana na utekelezaji na usimamizi mzuri wa ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi CCM 2020-2025.

CPA Makala amesema hayo huko katika Skuli ya Sekondari Ole iliyopo Wilaya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba wakati alipofanya ziara ya kukagua mradi huo.

Alisema, Wananchi wa Kisiwa cha Pemba wana kila sababu ya kuziunga mkono juhudi hizo za Chama Cha Mapinduzi CCM kwani zimeonesha matokeo chanya katika maisha yao hasa katika Sekta ya Elimu.

Aidha, CPA Makala amempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa utekelezaji wa Ilani ya CCM.

Alisema, amefarijika kuwaona wanafunzi wakisoma katika mazingira mazuri na salama ambayo yanaakisi maendeleo ya Sayansi na Taknolojia katika dunia jambo ambalo linachangia wanafunzi kufaulu kwakiwango kizuri.

Aidha, amewataka wanajamii wa maeneo ya Ole kuilinda na kuihifadhi miundombinu hiyo ili iweze kuleta manufaa kwa vizazi vya sasa na baadae.

Awali, akitoa taarifa fupi ya jengo hilo Afisa Mdhamin Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Mwalimu Mohammed Nassor Salim alisema, jengo hilo la Skuli ya Sekondari Ole nikati ya majengo 13 ya Skuli za Gorofa Pemba zilizojengwa chini ya Uongozi wa Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

Alisema, jengo hilo la ghorofa tatu Lina jumla ya Madarasa 40 ya kusomea, Maabara ya Sayansi, Chumba cha Kompyuta, Maktaba, Ofisi na Vyoo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here