NAIBU Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Miundombinu Mhandisi Rogatus Mativila amezielekeza Ofisi za Wakuu wa Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kufanya tathimi ya utekelezaji ya mipango wa bajeti kwa nusu mwaka.
Mhandisi Mativila ameyasema hayo wakati akifunga kikao kazi cha maandalizi ya Mpango na Bajeti kwa mwaka 2025/2026 kwa Wataalamu toka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Ofisi za Wakuu wa Mikoa Mamlaka za Serikali za Mitaa kinachofanyika Jijini Dodoma.
“Hakikisheni mnafanya tathimini ya nusu mwaka ya utekelezaji wa mpango wa bajeti ili kujilidhisha na hali halisi ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2024/2025” alisema Mhandisi Mativila.
Alisema, lengo la Tathimini hii ni kuona maeneo yenye changamoto na yale ambayo bado hayajafikiwa ili kuongeza kipaumbele kwenye nusu ya pili au katika bajeti inayofuata yam waka 2025/2026.
Aidha, Mhandisi Mativila amezielekeza Ofisi za Mikoa na mamlaka za Serikali za Mitaa kwenda kusimamia utekelezaji wa maagizo ya Kamati za kudumu za Bunge.
“Kuna maelekezo na maagizo yalitolewa na kamati za kudumu za Bunge za TAMISEMI, LAAC na PAC hivyo mkayasimamie utekelezaji wake na kuwasilisha ofisi ya Rais TAMISEMI ifikapo mwezi februari mwaka 2025 kwaajili ya kujilizisha na utekelezaji wa maagizo hayo” .