CCM mtaa wa Mbwamaji wazindua kampeni kwa kishindo

0

Na Andrew Chale, Kigamboni

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mtaa wa Mbwamaji wamezindua kwa kishindo kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambapo Wananchi watapiga kura siku ya Novemba 27, mwaka huu nchini kote.

Uzinduzi huo umefanyika katika eneo la Maduka mawili huku viongozi mbalimbali wa kichama na Wananchi wamehudhuria kushuhudia sera za Mgombea Uenyekiti kwa CCM Yohana Luhemeja, aliyeongozana na wagombea nafasi ya Ujumbe akiwemo Masenga Kiwango, Zubeir Fuko, Christopher Mabwai, Naim Pazi na Fatma Sima ambao kwa pamoja wameomba kura kwa Wana Mbwamaji ilikufanikisha maendeleo ngazi ya Serikali ya Mtaa huo.

Awali, akinadi sera zake Mgombea Uenyekiti Yohana Luhemeja anayetumia kauli mbiu: “Haki na uadilifu, Yohana kwa maendeleo ya Mbwamaji- Uwajibikaji na uwazi, alisema, kipaumbele ni kujenga shule ya Msingi, Zahanati, barabara pamoja na kuchimba Visima viwili Kanda ya Maduka mawili ilikufikisha maji eneo hilo sambamba na kumalizia upimaji wa ardhi mtaa wa mbwamaji.

“Niwaombeni Wana Mbwamaji, nina uzoefu wa mtaa huu. Kura yenu Novemba 27, ni muhimu na itaniwezesha kusimamia Afya, Miundombinu, Elimu na Mazingira lakini pia kusimamia upatikanaji wa mikopo kwa makundi maalum ya Vijana na Wanawake”. aliaema Yohana katika kampeni hiyo.

Aidha, alisema Mtaa huo wa Mbwamaji una Kanda Sita (6), ambazo ni kwa Fundi Baiskeli, Kanisa la pili, Makondeko, Maduka mawili, Bamba na Mbwamaji dimbwini watahakikisha maendeleo yanafika kila kona na kila Mwananchi akinufaika.

Akizungumzia zoezi la upimaji Ardhi, alisema: “Zoezi la upimaji ardhi lipo kwa asilimia 70, zoezi hili nililianzisha mie na sasa naomba kura zenu ilikwenda kulimalizia.

Aliongeza kuwa, mtaa wa Mbwamaji una Zahanati moja (1 ) ila ipo mbari na Kanda ya Maduka mawili hivyo wataona utaratibu wa kusogeza Huduma hiyo muhimu.

“Mwaka 2014 hadi 2019 nilichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa mtaa huu wa Mbwamaji kwa muda wa miaka mitano (5)
Nilifanya mengi:

.. ikiwemo kujenga Ofisi ya mtaa vyumba 3 na kufufua visima ikiwemo kisima cha maji kilichopo Gezaulole.

Pia, kuchonga barabara 36 za mtaa, nilitoa dawa na vifaa tiba Zahanati ya Gezaulole zenye thamani ya shilingi milioni 4.

Nilikuwa na utaratibu wa kuitisha mikutano ya Wananchi kila baada ya miezi mitatu (3) na hii ilisaidia sana maendeleo ya Mbwamaji, naombeni kura zenu Novemba 27 kuendeleza hili” Amesema Yohana Luhemeja.

Na kuongeza kuwa:
“Nilisimamia Ulinzi na Usalama, Usafi wa mazingira ndani ya mtaa na yapo mengi niliyo fanya ndani ya Uongozo wangu” amemalizia Yohana Luhemeja.

Aidha, mkutano wa mwisho wa kampeni unatarajiwa kufanyika Novemba 26, mwaka huu katika uwanja wa Mgudi Mbwamaji-Gezaulole huku akiwaomba Wananchi kujitokeza kwa wingi kusikiliza sera za Chama Cha Mapinduzi CCM.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here