Na Mwandishi Wetu
KATIKA mwaka 2024/25, Ofisi ya Rais – TAMISEMI imepanga kutumia Shilingi Bilioni 841.19 kwa ajili ya ujenzi, matengenezo, ukarabati wa miundombinu ya barabara na usafiri na usafirishaji wa vijijini na mijini ikiwamo ujenzi wa mifereji ya maji ya mvua yenye urefu wa Mita 141,070.54 na ujenzi wa kingo za Mto Msimbazi ili kudhibiti maeneo ya juu ya Mto Msimbazi.
Pia, kuhamisha karakana ya mabasi yaendayo haraka kutoka Jangwani kwenda eneo la Ubungo Maziwa.
Haya yamebainishwa bungeni na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI wakati wa kuwasilisha makadirio ya mapato na matumizi kwa Wizara hiyo, Sekretarieti za mikoa na mamlaka za serikali za mitaa na taasisi zake.
Alisema, kati ya fedha hizo Shilingi Bilioni 257.03 ni za Mfuko wa Barabara, Shilingi Bilioni 127.50 Mfuko Mkuu wa Serikali, Shilingi Bilioni 325.77 ni za tozo ya mafuta ya petroli na dizeli ya Shilingi 100 kwa lita, Shilingi Bilioni 4.03 za mapato ya ndani kupitia Wakala ya Mabasi Yaendayo Haraka Dar es Salaam na Shilingi Bilioni 126.85 ni fedha za nje.
Mchengerwa amebainisha shughuli ambazo zitakazotekelezwa kuwa ni utunzaji wa barabara za vijijini na mijini zenye urefu wa KM. 20,745.31, ujenzi wa barabara za lami zenye urefu wa Kilomita 434.50, ujenzi wa barabara za changarawe zenye urefu wa kilomita 13,802.34, ujenzi wa madaraja 160 na ukarabati wa madaraja 21 na ujenzi na matengenezo ya boksi kalavati 586 na vivuko 15.
Pia, kuboresha Miundombinu Shindanishi katika Miji Tanzania (TACTIC) kwa kujenga miundombinu katika Halmashauri 12 za Majiji ya Dodoma, Arusha, Mwanza na Mbeya na miundombinu msingi inajumuisha ujenzi wa masoko, mitaro ya maji ya mvua, stendi za mabasi, maghala ya kuhifadhia mazao na kujenga barabara kiwango cha lami kilomita 147.5.
Vilevile, kuondoa vikwazo vya barabarani kwenye wilaya 131 na ujenzi wa barabara kiwango cha lami Awamu ya Pili kilomita 164 kupitia Programu ya Kuongeza Fursa za Kiuchumi na Kijamii Nchini (RISE), uj