Dkt. Mwinyi ahimiza nidhamu, uadilifu na mshikamano

0

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amehimiza suala la nidhamu, maadili, uwajibikaji, uadilifu, mshikamano, umoja na upendo baina ya viongozi na watendaji wa Serikali katika kutenda haki kwa wananchi.

Rais Dkt.Mwinyi alisema hayo katika Kongamano la Kiimani kwa Viongozi na Watendaji Wakuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar lililoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais na kuratibiwa na Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar ukumbi wa Idrissa Abdul-Wakil Kikwajuni, Mkoa wa Mjini Magharibi Aprili 6, 2024.

Aidha Rais Dkt.Mwinyi alisema, suala la nidhamu sio kwa Majeshi peke yake ni suala la utumishi wa umma mzima.

Kwa upande mwingine Rais Dkt.Mwinyi alisema ili kuwepo uwajibikaji, maadili na nidhamu jambo kubwa ni kuwa na hofu ya Mungu na kuchunga ahadi zinazotolewa ili kutekeleza wajibu kwa uadilifu.

Rais Dkt.Mwinyi alisema, kongamano lijalo waalikwe Wenza wa viongozi na watendaji wa Serikali ili wapate kujifunza mada zinazotolewa na Masheikh na Wahadhiri.

Vilevile, Rais Dkt.Mwinyi alisema kodi ndiyo inayoendesha Serikali kwa kutekeleza huduma mbalimbali za kijamii , suala la kulipa kodi ni halali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here