Umoja wa Ulaya walaumiwa kwa kunyamazia mauaji Iraq

0

MICK Wallace, Mbunge wa Bunge la Umoja wa Ulaya ameulaumu umoja huo kwa kunyamaza kimya wakati askari wa jeshi la Marekani walipowaua kwa umati raia wa Iraq.

Wallace, ameandika ujumbe katika ukurasa wake wa Twitter wakati alipochangia ujumbe wa twitter uliozungumzia uhalifu na jinai zilizofanywa na jeshi la Marekani dhidi ya raia nchini Iraq.

“Kwa nini Umoja wa Ulaya haukutaka Marekani iwekewe vikwazo kutokana na mauaji ya halaiki iliyofanya nchini Iraq?”

Kuhusu jinai zilizofanywa na Marekani kwa kushirikiana na Shirika la Kijeshi la NATO dhidi ya raia wa Asia Magharibi, Wallace alisema: “kwa msaada wa wanachama wengine wa NATO, Marekani iliua zaidi ya raia Milioni Moja katika shambulio haramu na la kinyume cha sheria la kijeshi dhidi ya Iraq, na hadi sasa haujatolewa wito wowote wa kumwekea vikwazo mtu yeyote kwa ugaidi huu…”.

Katika mfululizo wa jumbe za ‘twitter’ zilizowekwa mtandaoni na mbunge huyo wa Bunge la Ulaya kuna picha zinazowaonyesha askari wa Marekani nchini Iraq wakiwa kando ya maiti kadhaa za raia wa nchi hiyo.

Tayari Umoja huo na Marekani wameiwekea vikwazo Urusi baada ya kuishambulia kijeshi Ukraine.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here