Ufunguzi wa Ubalozi wa UAE kuchochea utekelezaji wa miradi ya maendeleo

0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi akizungumza na mgeni wake Balozi Mdogo wa Umoja wa Falme za Kiarabu anayefanyia Kazi zake Zanzibar (Konseli Mkuu). Saleh Ahmed Al Hemeiri, alipofika Ikulu kwa mazungumzo na kujitambulisha 21-11-2022, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar

Na Subira Ally

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema hatua ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kufungua Ubalozi mdogo hapa Zanzibar, itaendeleza kasi katika kukuza uhusiano na ushirikiano wa muda mrefu uliopo kati ya nchi hizo mbili.

Dk. Mwinyi alisema hayo Ikulu Zanzibar, alipozungumza na Konseli Mkuu wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Saleh Ahmeid Alhemeir aliefika kwa ajili ya kujitambulisha.

Alisema hatua ya nchi hiyo kufungua Ubalozi mdogo hapa Zanzibar kutatoa msukumo katika utekelezaji wa miradi mbali mbali ya maendeleo ilioanzishwa pamoja na ile inayolengwa kuanzishwa siku za usoni.

Alisema ni matarajio yake kuwa kupitia Konseli Mkuu Alhemeir, miradi mbali mbali inayotekelezwa na nchi hiyo kupitia taasisi na Mashirika ya fedha ya nchi hiyo itafanikishwa.

Nae, Konseli Mkuu wa Umoja wa Falme za Kiarabu hapa Zanzibar Saleh Ahmeid Alhemeir alisema hatua ya UEA kufungua Ubalozi mdogo hapa Zanzibar itaaongeza kasi ya mahirikiano na hivyo akaahidi kufuatilia miradi mbali ambayo nchi hiyo imelenga ikisaidia Zanzibar.

Aidha, alisema atahakikisha anasimamia kikamilifu ujenzi wa Ofisi za Ubalozi mdogo wa nchi hiyo hapa Zanzibar.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here