Madaktari bingwa 12 kutoa huduma Hospitali ya Rufaa Iringa

0

Na WAF- DOM

SERIKALI Kupitia Wizara ya afya inaelekea kukidhi kiu ya Wananchi wa Mkoa wa Iringa kwa kupeleka kusoma jumla ya madaktari 12 watakaotoa huduma katika fani mbalimbali katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel leo Novemba 8, 2021 katika kikao cha bunge, Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Nancy Hassan Nyalusi Mbunge wa viti maalumu. 

Alisema, Katika kuongeza idadi ya madaktari bingwa, Wizara imepeleka kusoma jumla ya madaktari kumi na mbili (12) kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Iringa ambao watasaidia kuboresha huduma kwa wananchi wa Mkoa huo.

Akifafanua hilo Dkt. Mollel alisema, madaktari hao ni pamoja na; madaktari wawili wanasomea kinywa, sikio na koo, madaktari bingwa wa mifupa wawili, daktari wa magonjwa ya dharura mmoja, madaktari bingwa wa Watoto wawili, madaktari bingwa wa magonjwa ya ndani wawili, daktari bingwa wa meno mmoja, daktari bingwa wa usingizi mmoja na daktari bingwa mbobezi wa masuala ya Watoto mmoja. 

Aidha, Dkt. Mollel alisema, hadi sasa Hospitali hiyo ina jumla ya madaktari bingwa kumi na moja 11, madaktari bingwa wa afya ya akina mama na uzazi wanne, madaktari bingwa wa upasuaji wawili, daktari bingwa wa magonjwa ya ndani mmoja, daktari bingwa wa Watoto wawili, daktari bingwa wa macho mmoja na daktari bingwa wa mionzi mmoja.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here