📍 PWANI
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Pwani, imefanikiwa kukamata gari lililokuwa likisafirisha mafuta ya kupikia yaliyoingizwa nchini kinyume na sheria.
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo, tarehe 03/05/2026, majira ya saa 9 usiku katika eneo la Vikawe-Kibaha.
Katika tukio hilo, gari aina ya Toyota Chaser lilikamatwa likiwa na jumla ya madumu 50 ya mafuta ya kupikia, yaliyoingizwa nchini kwa njia ya magendo bila kufuata taratibu za kisheria.
Aidha, gari pamoja na mzigo wake vimehifadhiwa katika yadi ya Forodha Bagamoyo, kwa ajili ya uchunguzi zaidi huku hatua za kisheria na kiforodha zikiendelea kuchukuliwa dhidi ya wahusika.
TRA imendelea kusisitiza dhamira yake ya kudhibiti magendo na kuhakikisha wafanyabiashara wote wanafuata sheria na taratibu za kodi, ili kulinda uchumi wa nchi na kuhakikisha ushindani wa haki katika soko.