Na Sixmund Begashe, Njombe
TIMU ya Mchezo wa kuvuta kamba ya Wanaume na wanawake ya Wizara ya Maliasili na Utalii imeiburuza bila huruma timu pinzani za Utamaduni na Mashtaka 2-0 katika michezo ya Mei Mosi iliyoanza kurindima Mkoani Njombe.
Akizungumza baada ya michuano hiyo, Mwenyekiti wa Maliasili Sports Club Elia Mutalemwa amesema kuwa, siri ya ushindi huo ni maandalizi mazuri chini ya uangalizi wa viongozi wa Wizara.
Kocha wa timu hiyo Gabriel Michael amefafanua kuwa ushindi wa 2-0 wa timu ya Maliasili Wanawake Kamba dhidi ya timu ya Utamaduni, ulikuwa mwepesi kwao kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanyika kwa wachezaji wake.
Amewashukuru wakazi wa Njombe kwa kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu yao jambo lililo inua ari kubwa kwa wachezaji na kuipelekea pia timu ya Maliasili Wanaume kuiburaza bila huruma 2-0 timu ya Mashtaka na kuifanya iondoke uwanjani kwa majonzi makubwa.
Naye Neema Mkinga mkazi wa Makambako amesema amevutiwa na Michezo hiyo hasa namna timu zilivyojipanga hususan timu za Maliasili na Utalii.
Michuano hiyo ya kuelekea maadhimisho ya Sikuku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) yameanza rasmi Mkoani Njombe huku kila timu ikijigamba kuibuka na ushindi thidi ya timu nyingine.