BODI ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe, Balozi Valentino Mlowola, inaendelea na ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya mawasiliano iliyotekelezwa na UCSAF katika Mikoa ya Songwe na Mbeya.
Ziara hiyo imeanza rasmi jana, Januari 27, 2026, katika Mkoa wa Songwe. Kabla ya kuanza shughuli za ukaguzi wa miradi, Bodi ilifanya ziara ya heshima katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Jabiri Makame.
Katika siku ya kwanza ya ziara hiyo, Bodi imetembelea na kukagua minara ya mawasiliano iliyojengwa katika Kata ya Ifyekenya na Kata ya Ruanda, mkoani Songwe.