Uchaguzi usitutoe kwenye misingi ya kulienzi Taifa letu – Mbeto

0

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

WATANZANIA wametakiwa kutunza tunu ambazo zimeachwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ambazo ni umoja na amani na kuhakikisha uchaguzi unaotarajia kufanyika Oktoba 29, 2025 unapita salama.

Hayo yamesemwa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar, Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo Khamis Mbeto Khamis na kusisitiza, uchaguzi unafanyika kila baada ya miaka mitano, hivyo haupaswi kuwatoa watanzania kwenye misingi ya kulienzi Taifa.

Alisema, Taifa likiparaganyika, hakuna sehemu nyingine ambayo watanzania watakimbilia na kuwasihi wananchi wenye sifa kujitokeza kupiga kura uchaguzi utakapofika.

Aidha, Mbeto aliwataka watanzania kumuenzi baba wa Taifa kwa vitendo kwa kukemea maovu yote; rushwa, ubadhirifu na uhujumu uchumi.

“Hivi vyote ni adui wa haki, tusimamie kwenye haki na tueleze ukweli ili kulisaidia Taifa letu, kuna maisha baada ya uchaguzi,” alisisitiza Mbeto.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here