Dkt. Samia kuimarisha sekta ya madini, wachimbaji wadogo kuneemeka

0

MGOMBEA wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mwenyekiti wa CCM, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema iwapo atachaguliwa kwa awamu nyingine, ataimarisha zaidi sekta ya madini.

Ameyasema hayo wakati akijinadi kwenye mkutano wake wa kampeni uliofanyika Maganzo, Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Oktoba 11, 2025 na kuweka wazi kwamba, kipaumbele kitakuwa kwa wachimbaji wadogo.

Alisema, katika kipindi cha miaka minne iliyopita serikali ya Awamu ya Sita imeongeza utoaji wa leseni kwa wachimbaji wadogo wa madini hadi kufikia 1766 kutoka leseni 332 kama ilivyokuwa mwanzo.

Dkt. Samia amewapongeza wachimbaji wadogo wa madini ya Almasi katika eneo hilo pamoja na wachimbaji wote wadogo nchini kwa bainisha kuwa wameweza kuchangia asilimia 40 ya pato la madini nchini.

Aidha, amebainisha kuwa anafahamu kuhusu mgogoro uliopo katika Wilaya hiyo baina ya wamiliki wa mgodi, wananchi na wachimbaji wadogo kwa kuwahakikishia kuwa hatua zinachukuliwa na mgogoro huo utatatuliwa vema.

Aidha, akigusia kuhusu miundombinu ya barabara, Dkt. Samia ametangaza kuijenga upya barabara ya Kolandoto- Mwangongo, Manispaa ya Shinyanga kwa kiwango cha lami, mara baada ya kuwa inafanyiwa ukarabati wa mara kwa mara kwa muda mrefu.

Huu ni muendelezo wa mikutano yake ya kampeni ndani ya mkoa wa Shinyanga aliyoianza jana mkoani humo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here