Ujenzi wa jengo jipya la kisasa katika eneo la Kariakoo unaendelea kwa kasi chini ya ubia wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na Itel E.A Limited.
Jengo hili, lililopo katika Ploti Na. 9/28 na 10/28 katika barabara za Uhuru, Swahili na Aggrey, linajengwa kwa muundo wa B+G+11 na linatarajiwa kuwa kivutio kipya cha biashara na makazi katikati ya jiji.
Kazi zimehusisha ufungaji wa tiles kwenye stoo za ghorofa ya nne pamoja na kazi za chuma kwenye nguzo za ghorofa ya kumi.
Shughuli hizi zinaashiria kasi na umakini wa utekelezaji wa mradi kwa viwango vya juu vya ubora.
Pia, kikao cha wasimamizi wa mradi kimefanyika kujadili maboresho ya usalama kazini, usakinishaji wa mifumo ya kuzima moto, ubora wa kazi, uwasilishaji wa nyaraka muhimu, vipimo na uidhinishaji wa vifaa, pamoja na maendeleo ya jumla ya ujenzi.
Kupitia ubia huu, NHC na Itel E.A Limited wanaendeleza dhamira ya kuibadilisha sura ya Kariakoo na kuleta fursa mpya za kisasa kwa biashara na makazi bora.